Bank of Baroda Tanzania Limited (kifupi: BBTL) pia inajulikana kama Bank of Baroda Tanzania, ni benki ya biashara nchini Tanzania. Ni moja ya benki za biashara zilizo na leseni ya Benki ya Tanzania, mdhibiti wa benki kitaifa.[1]
BBTL inahusika katika nyanja zote za benki ya biashara, pamoja na kutumikia mashirika makubwa biashara ndogo na za kati na watu binafsi. BBTL ni kampuni ndogo ya Benki Ya Baroda (BOB), benki ya kimataifa yenye makao makuu nchini Mumbai, India. [2] Kuanzia tarehe 31 Disemba 2017, BBTL ilikua na vitu vya thamani ya bilioni 170 za kitanzania.[3] Kuanzia tarehe 31 Disemba, mtaji wake ulikua shillingi bilioni 35.33 za kitanzania.[2]
Historia
Benki hii ilifungua tawi lake la kwanza Tanganyika mnamo 1956. Ilipofika 1967, benki ilikuwa na matawi kwenye kila moja ya miji ya Dar es Salaam, Mwanza na Moshi. katika Februari 1967, benki ilifanywa kitaifa.[2][4]
Oktoba 2014 BBTL ilianzishwa kama ruzuku ya Benki ya Baroda , na tawi moja Dar es Salaam.[4] Miaka mitatu baadae mnamo Agosit 2007 tawi la pili lilifunguliwa mkoani Arusha, tawi la tatu lilifunguliwa Dar es Salaam Juni 2013 na tawi la nne lilifunguliwa Mwanza Julai 2014.
Mtandao wa matawi
Kigezo:Pia, BBTL ilikuwa na mtandao wa matawi katika maeneo yafuatayo:
- Makao Makuu: 149/32 Barabara ya Ohio Sokoine Drive, Dar es Salaam
- Tawi la Soko la Kariakoo: Soko la Karikoo, 8/13 Mtaa wa Mafia, Dar es Salaam
- Tawi la Arusha: 12E Mtaa wa Goliondoi , Arusha na
- Tawi la Mwanza: 153T Mtaa wa Kenyatta, Mwanza[5]
Marejeo
|
Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Benki ya Baroda Tanzania kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
|