Chekoslovakia ilikuwa nchi ya mataifa na utamaduni mbalimbali. Mataifa makubwa yalikuwa Wacheki (51,5 % ), Wajerumani (23,4 %) na Waslovakia (14 %) pamoja na vikundi vikubwa kidigo vya Wahungaria, Waukraine, Waromani na Wapoland.
Mwaka 1938 dikteta Adolf Hitler wa Ujerumani alivamia sehemu za Ucheki. Slovakia ikawa nchi ya kujitegemea chini ya Ujerumani.
1945 baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia umoja wa Ucheki na Slovakia ukarudishwa chini ya usimamizi wa Urusi. Warusi walihakikisha ya kwamba Chama cha Kikomunisti kilipata serikali. Utawala wa kikomunisti ulidumu hadi 1989. Baada ya kuanguka kwa ukuta wa Berlin utawala huu ulikwisha mwisho wa mwaka 1989.
Pande zote mbili za Ucheki na Slovakia ziliona ugumu wa kupatana. 1991 Umoja ulimalizwa na nchi mbili zilitoka katika shirikisho la Chekoslovakia.
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Chekoslovakia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.