Gesi ni moja kati ya hali maada. Katika hali ya gesi atomi hazishikani pamoja kama gimba mango bali zaelea kwa mwendo huria.
Atomi na molekuli za gesi huelekea kusambaa na kukalia nafasi yote ambamo imewekwa. Gesi haina umbo wala mjao kamili. Inawezekana pia kukaza gesi kwa mfano ndani ya chombo na kupunguza mjao kwa njia hii.
Mjao wa gesi hutegemea halijoto na shindikizo. Kama halijoto inaongezeka na shindikizo haibadiliki mjao utaongezeka.
Elmenti na dutu nyingi zapatikana kwa hali ya gesi.
Kuhusu gesi inayotumiwa kwa kuichoma kwenye jiko au katika injini angalia gesi asilia.