Malipo ni pesa au kitu atoacho mtu kulipia kitu alichonunua au kazi au huduma aliyofanyiwa. Malipo pia yanaweza kuwa ya shukrani kwa mazuri aliyofanyiwa mtu
Msamiati wa malipo mbalimbali
Arbuni/Rubuni/Advansi/Chambele/Kishanzu - malipo ya kwanza ya kuzuia kitu kisiuzwe.
Utotole/Kiangazamacho/Machorombozi/Chorombozi Kiokozi - zawadi ya ugunduzi wa kitu au kushuhudia jambo linapofanyika mahali wakati fuluani.
Mrabaha - faida au pato linalotokana na biashara; pia malipo anayopewa mwandishi au msanii na kampuni iliyotoa kazi yake kila baada ya kipindi fulani cha mauzo.
Fola - malipo ya kumshika mtoto mchanga kwa mara ya kwanza.
Kipkasa/Kipamkono/Jazua/Ukonavi - malipo anayopewa biharusi aonwapo mara ya kwanza.
Kikunjajamvi - ada idaiwayo kwa wafanyabiashara au wakazi wa mabaraza ya kiasili na ya kizamani ambayo hujumuisha fedha au mali, kwa mfano: kondoo, mbuzi, kuku n.k.
Bakora - zawadi ambayo baba humpa fundi akitaka mwanawe afundishwe ufundi.
Haka - malipo ya kufidia kosa fulani katika mambo ya familia.
Mukafaa - malipo ya mshahara kwa mfanyakazi kutokana na faida iliyopatikana.
Honoraria - malipo apewayo mtu kama bahashishi kwa kazi maalumu aliyoifanya.
Kudu - malipo alipayo mwari kwa nyakanga kama adhabu kwa kukosa adabu alipokuwa unyagoni.
Mwago - malipo kwa mke wa kwanza mume anapooa mke wa pili.
Mbiru - malipo kwa serikali kutokana na mishahara ya wafanyakazi wake.
Zaka - moja ya kumi ya mapato ambayo waumini wa dini humtolea Mwenyezi Mungu kama shukrani.
Tapisho - malipo kwa ngariba kwa ajili ya utahirishaji.
Pango - kodi ya nyumba alipwayo mwenye nyumba baada ya kipindi fulani kulingana na makubaliano.
Rehani - malipo ya kitu kilichowekwa dhamana ili kukombolewa baadaye.
Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Malipo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.