Nakumatt ni mtandao wa maduka nchini Kenya. Ina maduka 18 kote nchini Kenya na inaajiri watu 3,200. Ina mipango ya kupanua maduka yake mpaka nchini Uganda, Rwanda na nchi nyingine za Afrika Mashariki.
Mnamo 23 Agosti 2008, Nakumatt ilifungua ghala yake ya kwanza nje ya Kenya katika Union Trade Center, mjini Kigali, Rwanda.[3]
Mauzo ya mwaka 2006 ilikuwa zaidi ya US $ 300m, iliyozidi kwa 150% ya mauzo ya mwaka uliopita.[4] Kampuni hii ilikuwa na madai ya kushiriki katika ukwepaji wa kulipa ushuru mwaka 2006, ingawa hadi sasa hakuna mashtaka yaliyopelekwa kortini.[5]
Nakumatt ni ufupisho wa Nakuru Mattresses.[6]
Ghala moja ya Nakumatt mjini Nairobi ilichomeka kwa moto mkubwa mnamo 28 Januari 2009, na kuua watu 25.
Marejeo
↑Afrika Mashariki 25-31 Agosti 2008 - Special Supplement
Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Nakumatt kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.