Nyuzilandi (kwa Kiingereza: New Zealand; kwa Kimaori: Aotearoa) ni nchi ya visiwani katika Pasifiki takriban km 1,500 upande wa mashariki-kusini wa Australia.
Eneo lake linaundwa na visiwa viwili vikubwa: Kisiwa cha Kaskazini (North Island au Te Ika-a-Māui) na Kisiwa cha Kusini (South Island au Te Waipounamu) na vingine 600 vidogo.
Jiografia
Miji
Miji mingine ni:
Watu
Idadi ya wakazi ni 4,690,000. Wengi wao (74%) bado wana asili ya Ulaya, ingawa asilimia yao inazidi kupungua. Wakazi asilia ni Wamaori waliotokea Polinesia na kuhamia visiwa hivyo kati ya miaka 1250-1300 BK; kwa sasa ni 14.9% ya wakazi wote. Wengine wana asili ya Asia (11.8%) na ya visiwa vya Pasifiki (7.4%).
Lugha rasmi ni Kiingereza, Kimaori na Lugha ya Ishara ya Nyuzilandi (kwa Kiingereza: New Zealand Sign Language au NZSL).
Upande wa dini, 49% ni Wakristo wa madhehebu mbalimbali, kuanzia Kanisa Katoliki (12.6%), Anglikana (11.8%) na Wapresbiteri (8.5%). Idadi ya wasio na dini inazidi kupanda na imeshafikia 38.55%, mbali ya 12.27% wasiojibu swali kuhusu hilo. Kuna Mabanyani (2.1%), Wabuddha (1.5%), Waislamu (1.2%), Singasinga (0.5%)
Tazama pia
Viungo vya nje
|
Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.
Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.
|