Mwezi wa Oktoba ni mwezi wa kumi katika Kalenda ya Gregori. Jina lake limetokana na neno la Kilatiniocto, maana yake ni "nane", kwa vile katika kalenda ya kale ya Warumi, mwezi huo ulikuwa wa nane. Mwaka wa 153KK lakini, mwanzo wa mwaka ulitanguliza miezi miwili kutoka Machi kwenda Januari, na maana ya jina lake Oktoba ilipotea.
Oktoba ina siku 31, na inaanza na siku ya juma sawa na mwezi wa Januari ila katika miaka mirefu yenye siku 366.