Hii ni orodha ya vyuo vikuu katika nchi ya Malaysia. Vyuo vikuu hivyo ni vya aina mbili; yaani vyuo vya umma au serikali na vyuo vya binafsi. Vyuo vya binafsi vinajumuisha matawi ya vyuo vikuu vya Malaysia na kampasi za vyuo vya nchi za kigeni.
Orodha inayofuata imeainishwa katika matawi mawili ambayo yanaambatanishwa na majimbo vinamopatikana. Kwa kusudi la orodha hii, taasisi za masomo ya juu zilizoidhinishwa kutoa shahada za digrii lakini ambazo si vyuo vikuu zimejumuishwa katika mgao wa vyuo ambatani (ikiwa ni pamoja na taasisi zisizokuwa za elimu chini ya sheria ya elimu 1996).[1] Taasisi za masomo ya juu ambazo hazijaidhinishwa kuwapa shahada wanafunzi, zimeorodheswa katika orodha tofauti.
Ikiwa taasisi fulani hazina tafsiri rasmi ya majina yake, hupewa tafsiri na Muungano wa Jumuiya ya Vyuo Vikuu[2]na kutumiwa.
Vyuo vikuu na vyuo vingine vya umma
Vyuo vya umma nchini Malaysia hupata fedha kutoka kwa serikali na kutawaliwa/simamiwa kama taasisi za binafsi. Kando na Chuo Kikuu cha Malaysia na Chuo Kikuu Teknolojia cha Mara vilivyoanzishwa na sheria mbili tofauti za Bunge[3][4], vyuo vingine vya umma nchini Malaysia viliundwa na halmashauri kuu kutokana na sheria ya mwaka 1971 kuhusu vyuo vikuu na sehemu ya vyuo hivyo. Archived 20 Agosti 2008 at the Wayback Machine. Hadi hivi karibuni, Wizara ya Elimu iliwajibika kwa taasisi saba zilizo sehemu ya vyuo vikuu. Taasisi hizi (matawi ya vyuo vikuu) zimepandishwa daraja na kuwa vyuo vikuu na kwa sasa hamna matawi ya vyuo vikuu.
Vyuo vikuu na vyuo vingine vya binafsi
Kuanzishwa kwa vyuo vikuu vya binafsi na matawi ya vyuo vikuu kuliwezekana kutokana na sheria ya 1996 iliyoruhusu kuanzishwa kwa taasisi za elimu ya juu za kibinafsi. Archived 29 Oktoba 2008 at the Wayback Machine. Hapo awali taasisi za elimu ya juu za kibinsfsi zilikuwepo lakini hazikuidhinishwa kutoa shahada zake za digrii. Badala yake, ziliwapa wanafunzi mafunzo na kuwapa shahada kutoka vyuo vingine.
Marejeo
Angalia pia
Viungo vya nje