Mipaka yake na Uhindi na Uchina haitambuliki kimataifa. Pakistan na Uhindi zote mbili zinadai eneo la Kashmir zikitawala kila moja sehemu za eneo hili.
Jina la Pākistān lina maana ya "nchi ya watu safi" kwa Kiurdu.
Pakistani ina nafasi ya sita kati ya nchi duniani zenye watu wengi.
Mwaka 1917 Uingereza ulitamka ya kwamba ulitaka kuelekea polepole hali ya kujitawala kwa Wahindi. Viongozi wa wenyeji hawakuridhika na mkasi wa mabadiliko. Chini ya uongozi wa Mahatma Ghandi mwendo wa kupigania uhuru bila mabavu ulipata nguvu. Ghandi alipigania hasa umoja wa Wahindu na Waislamu lakini alipingwa na viongozi wenye itikadi kali wa pande zote mbili.
Baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia Waingereza walikubali kujiondoa katika Uhindi. Swali kubwa lilikuwa kama nchi itabaki kama nchi moja au kama maeneo ya Waislamu yatajitenga.
Baada ya uhuru
Tarehe 14/15 Agosti1947 utawala wa Uingereza ulikwisha. Bara Hindi iligawanywa katika nchi mbili za Uhindi na Pakistan. Mgawanyo wa Uhindi ulikuja na vita na kumwaga kwa damu nyingi.
Tarehe 30 Januari1948 Ghandi mwenyewe aliuawa na Hindu mkali aliyemchukia kwa sababu alitaka usawa wa Waislamu na Wahindu.
Wakati ule ilikuwa nchi moja pamoja na Bangla Desh ya leo, lakini mwaka 1971 hizo pande mbili zilitengana baada ya vita kati yao.
1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Pakistan kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.