Sanamu ya Mt. Radim Gaudentius akimfuata Mt. Adalbert, Libice nad Cidlinou, Ucheki.
Radim (kutoka Kicheki ; kwa Kipolandi Radzim ; jina la kitawa : Gaudencius[ 1] , Gaudentius[ 2] ; Libice , leo nchini Ucheki 970 hivi – Gniezno , leo nchini Polandi , 14 Oktoba 1020 hivi) alikuwa askofu mkuu wa kwanza wa Polandi[ 3] , akiwa na makao makuu huko Gniezno tangu mwaka 1000 .
Kabla ya hapo alikuwa amemfuata kaka yake, Adalberto wa Praha , katika monasteri na katika umisionari kwa Waprusia , akashuhudia alivyochomwa kwa mikuki na Wapagani kadhaa, naye mwenyewe alifungwa gerezani [ 4] .
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu .
Sikukuu yake ni tarehe 11 Oktoba [ 5] .
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo
Attwater, D.: Slovník svatých, Vimperk 1993
Attwater, Donald and Catherine Rachel John. The Penguin Dictionary of Saints . 3rd edition. New York: Penguin Books, 1993. ISBN 0-14-051312-4 .
Bruno z Querfurtu : Život svatého Vojtěcha, Praha 1996
Kolektiv: Bohemia Sancta: životopisy českých světců a přátel Božích, Praha 1990
Kolektiv: Svatý Vojtěch, sborník k mileniu, Praha 1997
Michal Lutovský, Zdeněk Petráň: Slavníkovci ISBN 80-7277-291-0
Viungo vya nje
Virtual tour Gniezno Cathedral Archived 2020-07-17 at the Wayback Machine
Makala hii bado ni mbegu . Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari .