Uwanja wa michezo Moses Mabhida ni uwanja wa soka unapatikana Durban, KwaZulu-Natal nchini Afrika Kusini, uliopewa jina la Moses Mabhida, Katibu Mkuu wa zamani wa Chama cha Kikomunisti cha Afrika Kusini. Ni uwanja wa matumizi mengi. Uwanja huo unatumika kwa ajili ya hafla kadhaa, kama kuruka kwa bungee, matamasha, kriketi, mpira wa miguu, mazoezi ya gofu na mengine mengi.[1]
Ulikuwa ni moja ya viwanja vya michezo vilivyotumiwa kwa ajili ya Kombe la Dunia la FIFAmnamo mwaka 2010. Uwanja una uwezo wa kuingiza watu 55,500 na ulipanuliwa hadi 75,000.[2] uwanja huu upo karibu na uwanja wa Kings Park.[3].
Marejeo
|
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu. Je, unajua kitu zaidi kuhusu Uwanja wa michezo Moses Mabhida kama historia yake, uenezi au kanuni zake? Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
|