Uzazi ni mchakato wa kibiolojia ambao kiumbe hai kipya kinapatikana kutokana na kingine au vingine.
Uwezo wa kuzaa ni kati ya sifa kuu zinazotambulisha uwepo wa uhai; kila kiumbe hai kilichopo duniani kimetokana na uzazi. Inakadiriwa kwamba kiumbe hai kilichozaa vile vyote vilivyopo leo kiliishi miaka 3,500,000,000 hivi iliyopita.
Njia za uzazi
Kuna njia mbili za uzazi: ile isiyotegemea jinsia, na ile inayoitegemea.
Uzazi wa kijinsia huwa unadai mchango wa wazazi wawili ambao kila mmojawao anakichangia kiumbe hai kipya kwa asilimia 50 za chembeuzi zake.
Uzazi wa binadamu
Binadamu akiwemo kati ya mamalia anazaa kwa namna inayofanana hasa na ile ya wanyama hao. Hata hivyo, akiwa na akili na utashi, anatakiwa kuratibu silika yake kuhusu uzazi ili uendane na uwajibikaji.
Tobler, M. & Schlupp,I. (2005) Parasites in sexual and asexual mollies (Poecilia, Poeciliidae, Teleostei): a case for the Red Queen? Biol. Lett. 1 (2): 166-168.
Zimmer, Carl. Parasite Rex: Inside the Bizarre World of Nature's Most Dangerous Creatures, New York: Touchstone, 2001.
The Evolution of Sex: An Examination of Current Ideas Richard E. Michod and Bruce E. Levin, editors (1987) Sinauer Associates Inc., Publishers, Sunderland, Massachusetts ISBN 0878934596ISBN 978-0878934591
Michod, R.E. Eros and Evolution: A natural philosophy of sex (1994). Addison-Wesley Publishing Company, Reading, Massachusetts ISBN 0201442329ISBN 978-0201442328
Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Uzazi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.