Wamarakwet ni jina lililobadilishwa kutoka Markweta. Ni kabila dogo katika kabila kuu la Wakalenjin: idadi yao ikikadiriwa kuwa 200,000. Inajumuisha makabila madogo ya Almoo, Cherangany (Sengwer au Kimaala), Endoow, Markweta (kabila dogo linalolipa jina lake la kawaida), Sombirir (Borokot) na Kiptaani ambao wanaishi kwa wingi katika kaunti ya Elgeyo-Marakwet eneo la Kaskazini mwa Bonde la Ufa nchini Kenya. Wengine wao wanaishi katika kaunti za Trans Nzoia Mashariki na Uasin Gishu Kaskazini na miji mingine nchini Kenya. Wachache wamekwenda kuishi katika maeneo ya mbali kama vile Afrika Kusini, Australia na hata Tennessee / Washington / New York nchini Marekani.
Sehemu inayokaliwa na Wamarakwet ndiyo mojawapo wa sehemu za kupendeza sana na maumbile mazuri nchini Kenya, ikipakana kwa sehemu ya mashariki Mto Kerio ukiwa mita 1000 juu ya usawa wa bahari, unaopitia katika sehemu ndogo ya Bonde la Ufa. Katika sehemu ya magharibi, inajumuisha sehemu yote ya milima ya Cherang’any ambayo urefu wake ni mita 3 300 juu ya usawa wa bahari magharibi mwa sehemu ya vilima ya Marakwet.
Makau makuu ya iliyokuwa Wilaya ya Marakwet ilikuwa katika mji ulio kwenye mlima wa Kapsowar. Sehemu nyingine za soko/miji ni Chebiemit, Kapcherop, Cheptongei, Arroor, Chesongoch, Chesoi, Kapyego, Tot, Sangach na Embobut Mosop.
Lugha
Wamarakwet huongea lugha ya Kimarkweta, ambayo inajumuisha Endow (Endoo), Kimala, Markweta na Sombirir na kadhalika.
Dini ya jadi
Dini ya kiutamaduni ya Wamarakwet ilijumuisha miungu mingi ikiwa na uwezo na mamlaka ya kutofautiana. Mungu wao muhimu alikuwa Assis (jua), wakati mwingine alijulikana kama Chebetip chemataw. Alitambulika sanasana na baraka na heri. Mungu wao mwingine ni Ilat (mungu wa ngurumo za radi). Alitambulikana na mvua na wakati wa kiangazi sadaka zilitolewa ili kumpendeza. Alitambulikana pia na hasira na kisasi kwani alisababisha kiangazi na kuchapa watu na radi akiwa amekasirishwa.
Maisha
Wamarakwet walijitenga katika vikundi/sehemu/makabila ambao hawakutambua mamlaka zaidi kuliko asiswo (mkusanyiko wa wanaume wote wa kundi hilo). Walijitenga katika miungano kulingana na sehemu zao za makazi kando ya Bonde la Kerio na kando ya Milima ya Cherangani.
Wao huishi maisha yanaojumuisha ukulima wa kujikimu pamoja na ufugaji wa ng'ombe za gredi, kondoo na kuku. Wao hupanda sanasana mahindi, viazi, maharagwe na mboga katika maeneo ya milima. Wale wanaoishi katika sehemu ya vilima na katika bonde la Kerio hukuza sana mbuzi na ng'ombe wa nyama ya zebu na hupanda mtama, wimbi, mihogo, mboga na matunda, haswa maembe na machungwa. Kuna mfumo usioeleweka wa kale sana wa kunyunyiza maji ya mitaro ambao hukimi mimea hiyo kando ya Bonde la Kerio ambao unaaminika kuweko kwa zaidi ya miaka 500.
Baadhi ya wakimbiaji wakuu wa masafa marefu, na haswa wa kuruka viunzi, duniani hutoka miongoni mwa kabila hili.
Vita
Makabila ya Wamarakwet na Wapokot ni matawi ya kabila kuu la Wakalenjin. Vita baina yao vilianza kwa sababu ya wizi wa mifugo, na tangu hapo kumekuwa na nyakati za vita na amani.
Vita vimekuwepo pia baina ya Wamarakwet kwa mfano, Kapkau na Karel kutoka bondeni kwa ajili ya mzozo wa mashamba na umesababisha vifo vya watu (11 waliuliwa Kapkau). Kulikuwa na maandamano na wakazi wa kata ya Sambirir kwa madai ya mauaji ya watu na kuiomba serikali kufanya operesheni katika sehemu za chini ili kuondoa bunduki zote lakini hakuna kilichofanyika. Mkuu wa Wilaya aliwahakikishia kuwa atafanya awezavyo ili kufanya Marakwet mahala pa amani.
Marejeo
- Marakwet of Kenya by Dr. Benjamin Edgar Kipkorir / F.W. Welbourn published in 1973 by the East African Literature Bureau.
- 'The Expansion of Marakwet Hill-Furrow Irrigation in the Kerio Valley of Kenya' by W. Ă–stberg. In Widgren, M. and Sutton, J.E.G. (eds.): Islands of Intensive Agriculture in Eastern Africa. James Currey publishers, Oxford, 2004 : 19-48.
Viungo vya nje
|
Makala hii kuhusu utamaduni wa Kenya bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Wamarakwet kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
|