Gianfranco Chiarini (alizaliwa Ferrara, 8 Januari 1966) ni mpishi kutoka nchini Italia, television personality na restaurateur. Anajulikana kote duniani kama mwanzilishi na balozi wa “Italian Nouvelle Cuisine” ambayo alitaka kuboresha upishi wa Kiitalia.
Ni mpishi wa teknolojia ya kisasa, mwandishi wa vitabu vya upishi na mwalimu. Mbali na hayo, Chiarini anafahamu lugha saba zikiwemo: Kiingereza, Kiitalia, Kihispania, Kifaransa, Kireno, Kijerumani na Kiarabu. Lugha hizi zimemwezesha kuwa mpishi anayevuka mipaka na kuzuru nchi mbalimbali na kufunza na kujifunza upishi mbalimbali duniani[1].
Maisha
Gianfranco Chiarini alizaliwa Italia, akiwa na asili ya Italia na Kolombia. Baba yake, Luciano Chiarini Toselli, ni mtaalamu wa Matangazo na Masoko na kwa sasa anayo kampuni yake ya masoko. Mama yake, Leonor Gonzales de Chiarini alikuwa mchezaji dansi wa nyimbo za classic ballet, na flamenco ila ajali mbaya barabarani ilikatiza ndoto yake ya kucheza ballet.
Amekulia katika nchi ya Italia, Venezuela na Marekani.
Alipotimiza miaka kumi na sita (16), Gianfranco aliondoka kwao kwenda kujitafutia riziki.
Mnamo 7 Septemba 2010, Chiarini alifunga ndoa na Anna Kinga Jarosławska ambaye alizaliwa Słupsk, Uholanzi na ni mtaalam wa vyombo vya habari na mkufunzi wa maandiko ya Kiitalia. Wote wawilli wameshirikiana kufanya biashara ya kusafirisha vyakula mbalimbali katika nchi za kigeni na pia za mbali. Katika hii biashara, Bwana Chiarini anazihusisha na nchi za nje kama vile Italia na bara Uropa. D.O.P na D.O.C mambo kama ya Kahawa, pasta, pesto, mvinyo, jibini, na vyakula vinginevyo. Bwana Chiarini na bibiye wanaishi nchini Hamburg, Germany, ingawa huko si nyumbani kwao, bali ndiko mahala wanapofanya biashara zao.
Muziki
Chiarini amewahi kucheza mziki hapo mbeleni. Mwanzoni aliichezea bendi la Rock vilabuni na vyumba vya vileo nchini Amerika. Chiarini alichoka na mambo ya miziki ya Rock na kuamua kurudia tamaduni za kilatino. Bwana Chiarini akajiunga na bendi nyingine kubwa la kispanyola iliyocheza nyimbo za salsa, “Band Barranco Mix”. Bendi hii ilijulikana katika nchi za uspanyola, na nchi zinginezo kama Amerika. Bendi hii ilicheza kwenye kipindi cha Johnny Canales huko Corpus Christi, Texas, pamoja na Malkia wa Tejano, Selena na bendi ya nyimbo za rock za kisasa Maná. Barranco ilikuwa bendi ya kwanza kulifungua Feria de Cali nchini Colombia. Wageni mashuhuri walishudia Salsa music zikichezwa. mwaka wa 1994 bendi hilo lilishinda tuzo tatu zitwazo Ronda awards, inayo fananishwa na Latin Grammy. Bendi hii ilitozwa tuzo la “best musical production”, “best young band of the year”, na kwa kuuza rekodi nying mwakani. Paukwa na hayo, ililituzwa tuzo la “double platinum” kwa kuuza zaidi ya rekodi millioni moja nchini Colombia, Mexico na Venezuela.
Pia ilijinyakulia kandarasi ya kurekodi nyimbo na Polygram Latino huko kaskazini mwa Amerika, Sonolux huko Colombia, Sonografica nchini Venezuela, Tele 5 nchini Uispania na bara zima la Europa. Chiarini aliiongoza bendi hili kwa nyimbo kutoka mwaka 1993 hadi 1996, kabla ya kujiunga na mambo ya upishi; aliyopenda zaidi.
Mwanzoni
Mnamo Mwaka 1986, kijana Chiarini alijiunga na chuo cha Instituto de Alta Gastronomia de Caracas, Venezuela. Chuo hiki kwa sasa kimefungwa kwa sababu ya mambo ya kisiasa. Wakati huo Chiarini alisoma pamoja na kufanya kazi katika mikahawa mbali mbali, ambapo aligundua kipawa chake cha upishi [2].
Kutokana na kuimba nyimbo mbali mbali za kilatino alijiwezesha kufanya masomo ya juu huko Amerika katika chuo cha Pittsburgh Culinary Institute (Culinary Institute of America) kinacho shirikiana na Le Cordon Bleu, mwaka wa 1996. Wakatii huu pia mambo hayakuwa tofauti alikuwa kwenye mikahawa na shule kama vile mbeleni. Wakati huu wote aliweza kuitumikia mikahawa kama The Ohio Brewery na Alberini’s. Alifanya kazi kama waiter, na mpishi huko Alberini’s siku zake za mapumziko aliendea kujifunza mbinu za karamu. Baada ya kutuzwa shahada kutoka chuo kikuu cha Pittsburgh Culinary Institute, alielekea Ufaransa ambapo palipo upishi wa kiwango cha hali ya juu duniani. Chiarini aliweza kujiunga na chuo kikuu cha Le Cordon Bleu Paris, chuo chenye mafunzo ya hali ya juu kote barani Europa.
Alipokuwa Le Cordon Bleu alifanya kazi na mababu wa upishi kama vile Alain Dutournier Mpishi na mkurugenzi mkuu wa mkahawa wa Carré des Feuillants, ** Michelin stars), kasha baadae Roma, Italy akifanya chini ya Mpishi mkuu Heinz Beck mkahawa wa La Pergola Restaurant , *** Michelin stars, Ferrara, Italy alifanyia mikahawa kama vile, Antichi Sapori na Hostaria Savonarola akiwa chini humo kama mpishi mkuu. Kisha akajiunga na mkahawa wa The Pirsch Mühle (* Michelin star), ujeremani hapa aliweza kufanya kazi ya upishi akishirikiana na Bwana, S. Leypold.
Ujuzi
Mwanzo wa milenia mpya Chiarini alimua kupeleka ustadi wake katika nchi za kigeni. Alielekea Uarabuni, hoteli ya kwanza zilikiwa Intercontinental huko Oman. Baadaye alijiunga na hoteli iitwayo Al Bustan Palace na Shangri-La Hotels. Baadaye alielekea nchini Bahrain, na kuinua hali ya upishi katika hoteli za kifahari za Mövenpick na Marriott hotels. Baadaye akasafiri nchini Kuwait, hapo akajiunga na hoteli za kifahari za Marriott Hotels kama mpishi Mkuu.
Nchini Kuwait Chiarini alikuwa rafikiye hayati Sheikh Jaber Al-Ahmad Al-Jaber Al-Sabah, Chiarini aliweza kulitengezea familia lake vyakula vya kifahari. Hapo ndipo sifa zake zilienea na kasha akaweza kuonesha ushupavu wake kwenye runinga la “Rai TV”. Chiarini alianza na zaidi ya vipindi 50 za upishi, Hapa aliweza kuonesha umaarufu wake na kuzileta upishi war barani uropa katika nchi za kiarabu. Hadi wa leo, Kuwait ndiyo nchi aipendayo zaidi.
Chiarini amendeleza upishi wake huko uispania, Bara europa na Bara Africa, Asia, Australia, New Zealand na Oceania. Huko Africa chiarini alifanya kazi katika hoteli za kifahari Starwood hotels, Mashariki mwa Africa; Sheraton Addis, ambayo ni moja yazo Starwood hotels. Ethiopia inajulikana kama nchiya ubalozi bara la africa, Sababu hio bwana Chiarini aliweza kukutana na marais wana siasa, mabalozi wa bara la Africa would cross.
Aliweza kutana naye Raisi wa 39th War nchi la Amerika, Jimmy Carter na bibiye Rosalynn Carter, Rais war nchi la Israel Shimon Peres, Na mwenye kiti war mashirika ya Afrika (AU) pamoja na rais war Misri Hosni Mubarak.
Alipokuwa bara la Asia aliweza kujifunza upishi wa mataifa kama Uchina, Korea, Cambodia, Vietnam, Thailand, Malaysia, Singapore na Uphilipino. Kuzuru kwake katika bala hilo limemfanya akaweza kujifunza upishi wa hali ya juu. Nako nchi za Australia, New Zealand and Oceania Sifa zake zimeenea tangu alipozindua kitabu chake cha kwanza litwalo “The New Renaissance of Italian Fusion Cuisine 1.0” Kitabu cha hali ya juu, kitabu hiki kiliweza kuwekwa kwenye kiwango cha hali ya juu na kuangazwa katika Mkahawa ilio bora duniani mzima iitwayo Noma . sifa za kitabu hiki zimeenea nchini kote Australia na vile vile njia za upishi za ki Italiano.Wakurugenzi wa kampuni la uchapishaji wa magazeti za upishi iitwayo food, wine and travel authority Visitvineyards.com walikiweka kitabu hiki kuwa kitabu moja ya vitabu kumi na mbili bora duniani mwaka wa 2010/2011.
Mwezi wa Januari 2011, Chiarini aliweza kuhojiwa na jet set magazine 8 (Thamāniya), kutoka Saudi Arabia. Hili ni Gazeti la familia lake Malkia Amira al-Taweel Naye Saudi Mkuu Al-Waleed bin Talal. Kando na hayo bwana chiarini ameweza kufanywa mpishi bora kwa ushujaa wake katika mambo ya upishi huko Uarabuni na kulichapisha kitabu cha “The New Renaissance of Italian Fusion Cuisine 1.0”.
Tanbihi
Marejeo
Tangu 2011, Mpishi Gianfranco Chiarini ameandika vitabu viwili (2) na ana panga kuandika Jumla ya vitabu 11 kabla ya mwaka 2021.
- Chiarini's "The New Renaissance of Italian Fusion Cuisine 1.0" The Emerald Book - Limited deluxe culinary trilogy edition (Nov-2010)
- Chiarini's "Ferrara the Hidden Culinary Jewel - Ferrara Il Gioiello Culinario Nascosto" Published in English/Italian (Sep-2011)
- Chiarini's "Ferrara the Hidden Culinary Jewel - Ferrara Il Gioiello Culinario Nascosto" Published in Malay/Italian (Sep-2011)
- Chiarini's "Ferrara the Hidden Culinary Jewel - Ferrara Il Gioiello Culinario Nascosto" Published in Japanese/Italian (Sep-2011)
- Chiarini's "Ferrara the Hidden Culinary Jewel - Ferrara Il Gioiello Culinario Nascosto" Published in Russian/Italian (Oct-2011)
- Chiarini's "The New Renaissance of Italian Fusion Cuisine 2.0" The Pearl Book - Limited deluxe culinary trilogy edition (Nov-2011)
Viungo vya nje
Tovuti rasmi
Nyingine
Makala