Share to: share facebook share twitter share wa share telegram print page

Imani ya Athanasio

Ngao ya Utatu inalenga kuonyesha mafundisho ya Imani ya Athanasio

Imani ya Athanasio (pia: Quicumque vult, kutokana na maneno ya kwanza ya Kilatini Quicumque vult salvus esse) ni mojawapo ya maungamo ya imani makuu ya imani ya Kikristo yanayokubaliwa katika makanisa ya magharibi, pamoja na Imani ya Mitume na Imani ya Nikea. [1] Inakazia mafundisho kuhusu Utatu wa Mungu na hali mbili za Yesu Kristo.

Historia ya matini

Katika mapokeo ya kanisa la magharibi, Athanasio wa Aleksandria (karne ya 4 BK) hutajwa kama mwandishi wa maungamo hayo. Maazimio ya Mtaguso wa Autun (mnamo 670 nchini Ufaransa) yalitaja mara ya kwanza "Imani ya Mtakatifu Athanasio" [2] na hapo inawezekana kwamba yalilenga matini ya "Quicumque".

Ila tangu karne ya 17 inajulikana kwamba matini hayo hayakutungwa na Athanasio[3]. Ni dhahiri kwamba ilitungwa kwa lugha ya Kilatini ilhali Athanasio hakutumia Kilatini akaandika kwa lugha ya Kigiriki. Vilevile matini yake yanakosa istilahi zilizokuwa muhimu kwa Athanasio kama vile homoousion, lakini inataja "Filioque" ambayo ni kawaida ya kanisa la magharibi ikikataliwa katika Ukristo wa Mashariki.[4] Pia ungamo hilo halijulikani katika Makanisa ya Mashariki, ingawa jina la Athanasius linaheshimiwa sana huko.

Inaonekana kwamba kwamba matini ya maungamo yaliunganishwa kwa kutumia nukuu kutoka kwa Mababu wa Kanisa la Kilatini (hasa mapokeo ya Augustino) kama vile Ambrosio wa Milan, Vincent wa Lérins, Fulgensyo wa Ruspe na hatimaye Caesarius wa Arles .

Muundo

Ungamo lina aya arobaini zilizogawanywa katika sehemu kuu mbili tofauti:

Matini kamili

Kilatini (kufuatana na Liber Usualis) Kiswahili (kufuatana na Tumwabudu Mungu Wetu)[5]

Quicumque vult salvus esse, ante omnia opus est, ut teneat catholicam fidem:

Kila atakaye kuokoka: Zaidi ya yote imemlazimu kuishika Imani Katholiko

Quam nisi quisque integram inviolatamque servaverit, absque dubio in aeternum peribit.

Ambayo, asipoihifadhi kamili na bila kuiharibu: bila shaka atapotea milele.

Fides autem catholica haec est: ut unum Deum in Trinitate, et Trinitatem in unitate veneremur:

Na Imani Katholiko ndiyo. hii: Tumwabudu Mungu mmoja katika Utatu, na Utatu katika Umoja.

Neque confundentes personas, neque substantiam separantes.

Tusizichanganye nafsi: Wala kuugawanya Uungu.

Alia est enim persona Patris, alia Filii, alia Spiritus Sancti.

Kwa maana Nafsi ya Baba mbali, Nafsi:ya Mwana mbali: Na Nafsi ya Roho Mtakatifu mbali.

Sed Patris, et Filii, et Spiritus Sancti una est divinitas, aequalis gloria, coeterna maiestas.

Bali Uungu wa Baba, na wa Mwana, na wa Roho Mtakatifu ni Uungu mmoja; Utukufu wao ni sawa, Ukuu wao ni wa milele.

Qualis Pater, talis Filius, talis Spiritus Sanctus.

Kama alivyo Baba, ndivyo alivyo Mwana: Ndivyo alivyo Roho Mtakatifu.

Increatus Pater, increatus Filius, increatus Spiritus Sanctus.

Baba hakuumbwa, Mwana hakuumbwa: Roho Mtakatifu hakuumbwa.

Immensus Pater, immensus Filius, immensus Spiritus Sanctus.

Baba hana mpaka, Mwana hana mpaka: Roho Mtakatifu hana mpaka.

Aeternus Pater, aeternus Filius, aeternus Spiritus Sanctus.

Baba ni wa milele, Mwana ni wa milele; Roho Mtakatifu ni wa milele.

Et tamen non tres aeterni, sed unus aeternus.

Walakini hakuna watatu walio wa milele: Bali Mmoja aliye wa milele.

Sicut non tres increati, nec tres immensi, sed unus increatus, et unus immensus.

Kadhalika hakuna watatu wasioumbwa, wala watatu wasio na mpaka: Bali asiyeumbwa ni mmoja tu, na asiye na mpaka ni mmoja tu.

Similiter omnipotens Pater, omnipotens Filius, omnipotens Spiritus Sanctus.

Kadhalika Baba ni Mwenyezi, Mwana Mwenyezi: Na Roho Mtakatifu Mwenyezi.

Et tamen non tres omnipotentes, sed unus omnipotens.

Walakini hakuna watatu walio Wenyezi: Bali aliye Mwenyezi ni mmoja tu.

Ita Deus Pater, Deus Filius, Deus Spiritus Sanctus.

Vivyo hivyo Baba ni Mungu, Mwana ni Mungu: Na Roho Mtakatifu ni Mungu.

Et tamen non tres Dii, sed unus est Deus.

Walakini hakuna Mungu watatu: Ila aliye Mungu ni mmoja tu.

Ita Dominus Pater, Dominus Filius, Dominus Spiritus Sanctus.

Vivyo hivyo Baba ni Bwana, na Mwana ni Bwana: Na Roho Mtakatifu

ni Bwana.

Et tamen non tres Domini, sed unus est Dominus.

Walakini hakuna Mabwana watatu: Bali Bwana ni mmoja tu.

Quia sicut singillatim unamquamque personam Deum ac Dominum confiteri christiana veritate compellimur: ita tres Deos aut Dominos dicere catholica religione prohibemur.

Kwa maana kama tunavyoshurutishwa kwa kanuni ya kweli ya Kikristo: Kukiri ya kuwa  kila Nafsi ni Mungu na Bwana. Kadhalika tunagombezwa na Imani Katholiko: Tusiseme ya kuwa wako Miungu watatu au Mabwana watatu.

Pater a nullo est factus: nec creatus, nec genitus.

Baba hakuumbwa na aliye yote: Hakuhulukiwa wala hakuzaliwa.

Filius a Patre solo est: non factus, nec creatus, sed genitus.

Mwana anatoka katika Baba tu: Hakuumbwa; wala hakuhulukiwa, bali yu Mwana wa azali.

Spiritus Sanctus a Patre et Filio: non factus, nec creatus, nec genitus, sed procedens.

Roho Mtakatifu anatoka katika Baba na Mwana: Hakuumbwa wala hakuhulukiwa, wala hakuzaliwa; bali anatoka.

Unus ergo Pater, non tres Patres: unus Filius, non tres Filii: unus Spiritus Sanctus, non tres Spiritus Sancti.

Basi yupo Baba mmoja tu, si Baba watatu; yupo Mwana mmoja tu, si Wana watatu: Yupo Roho Mtakatifu mmoja hu; si Roho Watakatifu watatu.

Et in hac Trinitate nihil prius aut posterius, nihil maius aut minus: sed totae tres personae coaeternae sibi sunt et coaequales.

Na katika Utatu huu hapana aliye wa kwanza na aliye wa baadaye: Hapana aliye mkuu zaidi na aliye mdogo. Bali Nafsi zote tatu ni wa milele: Wa sawa wote.

Ita ut per omnia, sicut iam supra dictum est, et unitas in Trinitate, et Trinitas in unitate veneranda sit.

Basi, katika mambo yote kama tulivyokwisha kusema: Imetupasa kuuabudu Umoja katika Utatu, na Utatu katika Umoja.

Qui vult ergo salvus esse, ita de Trinitate sentiat.

Kwa hiyo yeye atakaye kuokoka: Na aone hivyo juu ya Utatu.

Sed necessarium est ad aeternam salutem, ut Incarnationem quoque Domini nostri Iesu Christi fideliter credat.

Na zaidi ya hayo, ili apate wokovu wa milele: Imempasa kuamini kwa moyo Kufanyika mwili kwake Bwana wetu Yesu Kristo.

Est ergo fides recta, ut credamus et confiteamur, quia Dominus noster Iesus Christus Dei Filius, Deus et homo est.

Na Imani kamili ndio hii; Tuamini na kukiri ya kuwa Bwana wetu Yesu Kristo, Mwana wa Mungu, ni Mungu na Mwanadamu.

Deus est ex substantia Patris ante saecula genitus: et homo est ex substantia matris in saeculo natus.

Yu Mungu, ana Uungu wa Baba, yu Mwana kabla ya zamani zote: Ni Mwanadamu, ana utu wa mama yake, alizaliwa katika ulimwengu.

Perfectus Deus, perfectus homo: ex anima rationali et humana carne subsistens.

Mungu kamili na Mwanadamu: Ana roho yenye akili na mwili wa kibinadamu.

Aequalis Patri secundum divinitatem: minor Patre secundum humanitatem.

Yu sawa na Baba kwa kuwa ni Mungu: Yu chini ya Baba kwa kuwa

ni Mwanadamu.

Qui, licet Deus sit et homo, non duo tamen, sed unus est Christus:

Na ijapokuwa yu Mungu tena Mwanadamu: Yeye si wawili; bali ni Kristo mmoja.

Unus autem non conversione divinitatis in carnem, sed assumptione humanitatis in Deum:

Yeye ni mmoja, si kana kwamba Uungu umebadilika uwe mwili: Bali kwa kuutwaa utu wa mwanadamu na kuuunga na Mungu.

Unus omnino non confusione substantiae, sed unitate personae.

Mmoja kabisa, si kwa kuuchanganya Uungu na utu: Bali kwa kuwa Nafsi mmoja tu.

Nam sicut anima rationalis et caro unus est homo: ita Deus et homo unus est Christus.

Kwa maana kama vile nafsi yenye akili pamoja na mwili huwa mwanadamu mmoja: Kadhalika Mungu na Mwanadamu pamoja ni Kristo mmoja.

Qui passus est pro salute nostra, descendit ad inferos: tertia die resurrexit a mortuis.

Aliyeteswa kwa wokovu wetu: Akashuka mahali pa wafu, akafufuka

siku ya tatu.

Ascendit ad caelos, sedet ad dexteram Dei Patris omnipotentis: inde venturus est iudicare vivos et mortuos.

Akapaa mbinguni, ameketi mkono wa kuume wa Baba, Mungu Mwenyezi: Kutoka huko atakuja kuwahukumu waliohai na waliokufa.

Ad cuius adventum omnes homines resurgere habent cum corporibus suis: et reddituri sunt de factis propriis rationem.

Naye atakapokuja, wanadamu wote watafufuliwa na miili yao: Nao watatoa habari za matendo yao.

Et qui bona egerunt, ibunt in vitam aeternam: qui vero mala, in ignem aeternum.

Nao waliotenda :mema wataingia katika Uzima wa milele: Nao waliotenda mabaya katika moto wa milele.

Haec est fides catholica, quam nisi quisque fideliter firmiterque crediderit, salvus esse non poterit.

Hii ndiyo Imani Katholiko: Ambayo mtu asipoisadiki kwa uuaminifu  hawezi kuokoka.

Matumizi makanisani

Wakati wa Matengenezo ya Kiprotestanti imani hiyo ilihesabiwa kama moja ya maungamo makuu matatu yaliyotumiwa makanisani. Kanisa la Kiinjili la Kilutheri limelipokea kati ya maungamo yake na pia Wareformed wanalitambua.

Kwa sasa inatumika katika liturujia ya makanisa ya Kianglikana; liko pia katika kitabu cha "Tumwabudu Mungu wetu" wa KKKT.

Lilikuwa sehemu ya liturujia ya sala ya asubuhi ya saa 12 (prim) katika Kanisa Katoliki; tangu kuondolewa kwa utaratibu huo kutoka Liturujia ya Vipindi matini ya Quicumque vult yanatumika na wachache tu.

Tanbihi

  1. https://web.archive.org/web/20050429143510/http://www.vatican.va/archive/DEU0035/_P1B.HTM Katechismus der Katholischen Kirche, Artikel 193
  2. Hubert Mordek: Kirchenrecht und Reform im Frankenreich. Die Collectio Vetus Gallica, die älteste systematische Kanonessammlung des fränkischen Gallien. Berlin 1975, S. 84ff.
  3. O'Carroll, Michael (1987), "Athanasian Creed", Trinitas, Collegeville: Liturgical Press, ISBN 0814655955
  4. Norris, Frederick (1997), "Athanasian Creed", in Ferguson, Everett (ed.), Encyclopedia of Early Christianity (2nd ed.), uk. 110, New York: Garland, ISBN 0824057457, [https://archive.org/details/encyclopediaofea0000unse/page/110/mode/2up online hapa]
  5. Matini iliyochapishwa katika kitabu cha Tumwabudu Mungu Wetu 2012, kilichotolewa na KKKT, ISBN 9987-652-08-5
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Imani ya Athanasio kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Read other articles:

Các vụ đánh bom tại Ankara năm 2015Nhà ga AnkaraAnkaraAnkara (Thổ Nhĩ Kỳ)Địa điểmPhía trước nhà ga AnkaraTọa độ39°56′11″B 32°50′38″Đ / 39,9364°B 32,8438°Đ / 39.9364; 32.8438Thời điểm10 tháng 10 năm 201510:04 EESTMục tiêuThường dânLoại hìnhĐánh bom tự sát, Giết người tập thểTử vong109+[1](theo Hiệp hội Y tế Thổ Nhĩ Kỳ)Bị thương400+[1...

 

قرية نيو بالتز     الإحداثيات 41°45′00″N 74°05′00″W / 41.75°N 74.0833°W / 41.75; -74.0833  تاريخ التأسيس 1887  تقسيم إداري  البلد الولايات المتحدة[1]  التقسيم الأعلى مقاطعة أولستر، نيويورك  خصائص جغرافية  المساحة 1.8 ميل مربع  عدد السكان  عدد السكان 7324 (1 أبر

 

يفتقر محتوى هذه المقالة إلى الاستشهاد بمصادر. فضلاً، ساهم في تطوير هذه المقالة من خلال إضافة مصادر موثوق بها. أي معلومات غير موثقة يمكن التشكيك بها وإزالتها. (مارس 2016) العراق تحت 17 سنة منتخب العراق تحت 17 سنة لكرة القدم معلومات عامة بلد الرياضة العراق  الفئة كرة قدم تحت 17 سن...

Boca Gemeente in Italië Situering Regio Piëmont (PMN) Provincie Novara (NO) Coördinaten 45° 41′ NB, 8° 25′ OL Algemeen Oppervlakte 9,6 km² Inwoners (1 januari 2018) 1.213[1] (124 inw./km²) Hoogte 389 m Overig Postcode 28010 Netnummer 0322 Beschermheilige San Gaudenzio Naam inwoner bochesi ISTAT-code 003019 Portaal    Italië Boca is een gemeente in de Italiaanse provincie Novara (regio Piëmont) en telt 1195 inwoners (31-12-2004). De oppervlakte bedraagt 9...

 

Grady Diangana Diangana en 2019Datos personalesNacimiento República Democrática del Congo19 de marzo de 1998 (25 años)Nacionalidad(es) BritánicaCongoleñaAltura 1,80 m (5′ 11″)Peso 73 kg (161 lb)Carrera deportivaDeporte FútbolClub profesionalDebut deportivo 2016(West Ham United F. C.)Club West Bromwich Albion F. C.Liga EFL ChampionshipPosición CentrocampistaDorsal(es) 11Selección nacionalSelección COD República Democrática del CongoPart. (goles) 1 (...

 

Artikel ini hampir seluruhnya merupakan ringkasan alur. Artikel ini harus diperluas untuk menyediakan cakupan konteks dunia nyata yang lebih seimbang. Please edit the article to focus on discussing the work rather than merely reiterating the plot. (Pelajari cara dan kapan saatnya untuk menghapus pesan templat ini) Pocong Jumat KliwonSutradara Nayato Fio Nuala Produser Gope T. Samtani Subagio S Ditulis oleh Ery Sofid PemeranZacky ZimahMonique HenryLeylarey LesesneArumi BachsinDana ColeSazha Cl...

  لمعانٍ أخرى، طالع بوبي مور (توضيح). بوبي مور Bobby Moore بوبي مور عام 1969 معلومات شخصية اسم الولادة روبرت فريدريك تشيلسي مور الميلاد 12 أبريل 1941(1941-04-12)إسكس، إنجلترا، المملكة المتحدة الوفاة 24 فبراير 1993 (عن عمر ناهز 51 عاماً)لندن، إنجلترا، المملكة المتحدة سبب الوفاة سرطان ال�...

 

Le maillot jaune version 2004. Cet article présente les statistiques du classement général du Tour de France. Depuis le premier Tour de France en 1903, il s'est déroulé 2 235 étapes, en incluant la 21e étape du Tour de France 2023. Depuis 1919, le leader de la course porte à chaque étape un maillot jaune. Dans cet article, les leaders du classement général des Tours avant 1919 sont également comptabilisés comme si un maillot jaune leur avait été attribué. À not...

 

Town in Ontario, CanadaPerthTown (lower-tier)Town of PerthMotto(s): Pro Rege, Lege et GregePerthPerth in southern OntarioCoordinates: 44°54′N 76°15′W / 44.900°N 76.250°W / 44.900; -76.250CountryCanadaProvinceOntarioCountyLanarkSettled1816Incorporated1853 (Upper Canada Municipal Corporations Act, 1849)Government • TypeTown • MayorJudy Brown • Federal ridingLanark—Frontenac—Kingston • Prov. ridingLanark—F...

This article is part of a series on thePolitics ofMalaysia Head of State Yang di-Pertuan Agong Abdullah of Pahang Conference of Rulers Legislature Parliament of Malaysia 15th Parliament Senate (Dewan Negara) President Wan Junaidi Tuanku Jaafar House of Representatives (Dewan Rakyat) Speaker Johari Abdul Leader of the Government Anwar Ibrahim Leader of the Opposition Hamzah Zainudin Executive Cabinet Prime Minister Anwar Ibrahim Civil service (agencies) Chief Secretary Mohd. Zuki Ali Judiciary...

 

Character group from J. R. R. Tolkien's legendarium Dark Riders and Black Riders redirect here. For other uses, see Dark Rider (disambiguation), Black Rider (disambiguation), and Nazgul (disambiguation). Fictional character NazgûlIn-universe informationAliasesThe NineÚlairi (in Quenya)Black RidersFell RidersRingwraithsBook(s)The Fellowship of the Ring (1954),The Two Towers (1954),The Return of the King (1955),The Silmarillion (1977),Unfinished Tales (1980) The Nazgûl (from Black Speech naz...

 

2023 European ChampionshipsVenuePalacio Multiusos de GuadalajaraLocation Guadalajara, SpainDates22–26 MarchCompetitors535 from 47 nations← 2022 Gaziantep2024 Split → 2023 European Karate ChampionshipsMenWomenKataKata60 kg50 kg67 kg55 kg75 kg61 kg84 kg68 kg+84 kg+68 kgTeam kataTeam kataTeam kumiteTeam kumitevte The 2023 European Karate Championships was the 58th edition of the European Karate Championships and 5th European Para Karate Championships and we...

2011 filmThe EgoistsFilm posterDirected byRyuichi HirokiWritten byKenji NakagamiProduced byYasushi MinatoyaAkira Morishige[2]StarringAnne SuzukiKengo KoraSora AoiYasushi FuchikamiKaoru KobayashiMako MidoriJun MurakamiToshie NegishiNao OhmoriShûgo OshinariTomorō Taguchi[3]Release date 4 June 2011 (2011-06-04) Running time136 minutesCountryJapan[1]LanguageJapanese[4] The Egoists (Japanese: 軽蔑, Hepburn: Keibetsu, Scorn) is a 2011 Japanese dram...

 

Statue of Venus (modest Venus) For the chamber opera, see The Capitoline Venus (opera). The Capitoline Venus (Capitoline Museums). The Capitoline Venus is a type of statue of Venus, specifically one of several Venus Pudica (modest Venus) types (others include the Venus de' Medici type), of which several examples exist. The type ultimately derives from the Aphrodite of Cnidus. The Capitoline Venus and her variants are recognisable from the position of the arms—standing after a bath, Venu...

 

1961 song by Paul Frees as Ludwig Von DrakeThe Spectrum SongSong by Paul Frees as Ludwig Von DrakeReleased1961GenreDisney song, children's songComposer(s)Richard M. Sherman, Robert B. ShermanThe Spectrum Song was written by the Sherman Brothers in 1961 under assignment from Walt Disney to be a signature song for the fictional character Ludwig Von Drake. Nominally about different colors in the spectrum, the song's lyrics initially consist of the repeated color names red, yellow, green and blue...

1944 film by William Beaudine Follow the LeaderDirected byWilliam BeaudineScreenplay byWilliam BeaudineBeryl SachsStory byAnde LambProduced byJack DietzSam KatzmanStarringSee belowCinematographyMarcel Le PicardEdited byCarl PiersonProductioncompanyMonogram PicturesRelease date 1944 (1944) Running time65 minutesCountryUnited StatesLanguageEnglish Follow the Leader is a 1944 American film directed by William Beaudine featuring the East Side Kids.[1] Plot As he and Glimpy Freedhoff ...

 

Le Traité du gouvernement civil (Two Treatises of Government en anglais) est un essai philosophique rédigé par le philosophe anglais John Locke, publié en 1690, consacré à l’origine, à la légitimité et aux problèmes posés par tout gouvernement politique. Structure Comme l’indique son titre original en anglais, le Traité du gouvernement civil est en réalité composé de deux traités distincts, publiés à titre anonyme. Le premier a pour objet de « mettre en évidence e...

 

Le informazioni riportate non sono consigli medici e potrebbero non essere accurate. I contenuti hanno solo fine illustrativo e non sostituiscono il parere medico: leggi le avvertenze. Due marinai della US Navy in una camera di decompressione durante un addestramento. La camera di decompressione è un apparato in grado di sopportare la pressione di aria al suo interno (superiore a quella atmosferica, da cui il termine iperbarica) e che permette di ospitare persone che abbiano la necessità di...

Este artículo o sección tiene referencias, pero necesita más para complementar su verificabilidad.Este aviso fue puesto el 25 de febrero de 2021. Château d'Étampes monumento histórico clasificado y bien recensé dans l'Inventaire général du patrimoine culturel La Tour de GuinetteLocalizaciónPaís FranciaCoordenadas 48°26′14″N 2°09′30″E / 48.437222222222, 2.1583333333333Información generalEstado ÉtampesDeclaración 1862Inicio Siglo 11Finalización 1150Propi...

 

South Korean actor (born 1970) For other uses, see Lee Byung-hun (disambiguation). In this Korean name, the family name is Lee. Lee Byung-hunLee in November 2023Born (1970-07-12) July 12, 1970 (age 53)Seoul, South KoreaEducationHanyang UniversityOccupationActorYears active1991–presentAgentsUnited Talent AgencyBH (Kakao M)Spouse Lee Min-jung ​(m. 2013)​Children1Korean nameHangul이병헌Hanja李炳憲Revised RomanizationI Byeong(-)heonMcCune–Reischaue...

 
Kembali kehalaman sebelumnya