Jina hili lilianza kutumika kwa sababu kwa lugha ya Kigiriki lina maana ya namba50. Hivyo "πεντηκοστή [ἡμέρα]" (pentekostē [hēmera]) ni "(siku ya) hamsini".
Shavuot ya Kiyahudi
Sikukuu ya Kiyahudi ya Pentekoste inaadhimishwa siku ya hamsini baada ya Pasaka ya Kiyahudi. Sikukuu hii husherehekewa na Wayahudi pia kwa jina asili la Kiebrania חג השבועות, Hag ha Shavuot, yaani Sikukuu ya Majuma, kwa kifupi "shavuot" ("majuma") jinsi ilivyoamriwa katika kitabu cha Mambo ya Walawi 23:16.
Ilikuwa sikukuu ya mavuno kama vile Pasaka ilivyohusiana na malimbuko.
Inawezekana kusema ya kuwa baada ya kifo na ufufuko wa Yesu wanafunzi wake - ambao walikuwa wote Wayahudi - walikutana kwenye sikukuu ya Kiyahudi ya Shavuot wakati ambapo Wayahudi kutoka nchi mbalimbali walipotembelea Yerusalemu kwa hija kwenye nafasi ya sikukuu ile.
Humo Mwinjili Luka anasimulia jinsi wanafunzi wa Yesu walivyokutana katika mji wa Yerusalemu siku ile ya "Pentekoste" na kupokea paji la Roho Mtakatifu. Baadaye walitoka nje ya nyumba ya ghorofa walimokaa, wakianza mara kuhubiri juu ya Yesu Kristo mbele ya watu wengi, wakiwa wakazi wa mji huo pamoja na wageni kutoka nchi nyingi.
Kufuatana na taarifa yake siku hiyo watu takriban 3,000 walibatizwa kwa jina la Yesu na kuongezeka katika kile kikundi. Ndiyo maana Pentekoste inahesabiwa kuwa kuzaliwa kwa Kanisa.
Kuanzia mwaka 1907, katika Ukristo limejitokeza tapo la kiroho linalosisitiza umuhimu wa karama kama zilivyojitokeza siku ya Pentekoste na mwanzoni mwa Kanisa. Ndiyo sababu waumini wake wanaitwa Wapentekoste.
Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Pentekoste kama historia yake au athari wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.