Jina "Monduli" linasemekana kututoka kwa mmoja mzee wa Masai aliyeitwa "Monduli" na kukaa katika eneo la kata ya Monduli Juu wakati wa ukoloni wa Kijerumani.
Utawala
Wilaya ya Monduli ilikuwa sawa na Jimbo la Uchaguzi la Monduli wakati wa uchaguzi wa bunge. Eneo limegawiwa kwa kata 15 na 51 vijiji au mitaa ya mjini. Eneo lote ni kilomita za mraba 6,419.
Makao makuu ya wilaya iko Monduli Mjini ambayo ni moja wa miji midogo miwili (pamoja na Namanga) katika wilaya yenye tabia ya vijijini.
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Arusha bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Wilaya ya Monduli kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.