Kisiwa kina eneo la km² 2.512 kikiwa na kipenyo cha km 50 hadi 70.
Milima mikubwa ni ya kivolkeno. Upande wa mashariki wa kisiwa ndipo mlima wa "Piton de la Fournaise" wenye urefu wa mita 2611 uliolipuka zaidi ya mara 100 tangu kumbukumbu ya kimaandishi ilipoanzishwa mwaka 1640. Mlipuko wa mwisho hadi leo ulitokea tarehe 4 Oktoba2005.
Mlima wa "Piton des Neiges" ndio mkubwa kisiwani ikiwa na 3070 m juu ya UB.
Baadaye Wareno walitumia jina la nahodha maarufu Pedro de Mascarenhas na kujumlisha visiwa vya Reunion, Mauritius na Rodrigues kwa jina la visiwa vya Maskareni. Visiwa hivyo vilikuwa na umuhimu fulani kama vituo vya kupumzika katika safari kati ya Ulaya na Bara Hindi, mabaharia wakitafuta maji ya kunywa, nafasi ya kutengeneza jahazi zao na kuongeza chakula. Lakini hapakuwa na makao ya kudumu kisiwani.
Utawala wa Kifaransa
Mwaka 1640 Wafaransa walivamia kisiwa na kukitangaza kuwa mali ya Ufaransa. Walikiita "Île Bourbon" kutokana na jina la familia ya wafalme wa Ufaransa.
Mwaka 1768 kisiwa kilikuwa na wakazi huru 26,284 (hasa Wafaransa) na watumwa 45,000.
Ufaransa ulitia sahihi maazimio ya Mkutano wa Vienna mwaka 1815 pamoja na kumaliza biashara ya watumwa lakini biashara hii iliendelea kwa siri na kupanuka hasa kwa wafungwa kutoka Afrika. Idadi ya watumwa iliendela kuongezeka hadi kuondolewa hali ya utumwa tarehe 20 Desemba1848.
Baada ya mwisho wa utumwa walowezi walitafuta wafanyakazi huko Bara Hindi wakachukua Wahindi wasiofika kama watu huru kwa miaka na haki kidogo.
Mwaka 1946 Reunion ilipewa cheo cha Mkoa wa Ufaransa, na tangu 1997 imekuwa sehemu ya Umoja wa Ulaya.
Mkoa wa Reunion ina wilaya (Kifaransa: arrondissements) nne.
Wakazi
Wakazi wanaonyesha historia hii katika mchanganyiko wao wa aina za watu na tamaduni kutoka pande mbalimbali wa dunia.
Sehemu kubwa ya wakazi ni wajukuu wa watumwa au wafanyakazi wasio huru wa zamani wakionyesha tabia za Wahindi, Waafrika na Wachina. Takriban robo ya wakazi ni wa asili ya Ulaya.
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Réunion kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.