Mara nyingi Wagonde upande wa kusini wa mto Songwe nchini Malawi huhesabiwa pamoja nao katika kundi lilelile.
Mwaka 1993 watu zaidi ya milioni walikuwa wanajumlishwa kwa jina hili, takriban 750,000 upande wa Tanzania na 300,000 upande wa Malawi.
Historia
Kihistoria watu wanaoitwa leo Wanyakyusa waliitwa Wakonde, ambao kati yao Wanyakyusa walikuwa ndio kabila kubwa. Wakati wa karne ya 20 "Wanyakyusa" limekuwa jina la kundi kwa jumla.
Wakati Wajerumani walipofika sehemu za kaskazini kwa Ziwa Nyasa mwisho wa karne ya 19 hawakuona tofauti ya msingi kati ya watu wa Malawi kaskazini na wale wa sehemu za Rungwe wakawaita wote "Wakonde" kutokana na jina lililokuwa kawaida ziwani.
Mgawanyiko wa Wanyakyusa
Wanyakyusa toka zamani walijulikana kama watu wa Konde. Wengi walikuwa kaskazini kwa ziwa Nyasa, lakini katika harakati za maisha na mabadiliko ya mazingira wengi wao wakakimbilia Mbeyamjini na sehemu nyingine.
Pamoja na hayo, hasa Wanyakyusa wapo wa aina mbili nao ni: Wanyakyusa wa Tukuyu na Wanyakyusa wa Kyela.
Sifa za Wanyakyusa wa Kyela
1. Wengi si wapole mtu afanyapo kosa
2. Wanamcha Mungu
3. Wanajua kupenda
4. Hawapendi dharau
5. Wanapenda kujulikana (hasa kama wamesoma hadi kupata digrii n.k.)
6. Ni wapiganaji sana kimaisha
7. Wana wivu katika masuala ya mapenzi
8. Wanapenda haki itendeke, hawapendi ubabaishaji
9. Ni watu shupavu sana kwenye kazi za kujitolea, hasa za kijamii
Sifa za Wanyakyusa wa Tukuyu
1. Ni wapole
2. Wanamcha Mungu
3. Wanajua kupenda
4. Hawapendi dharau kabisa
5. Wanajituma kwenye kazi, hasa kilimo
6. Wana wivu sana
7. Wanapenda haki itendeke na hawapendi ubabaishaji
8. Ni watu jasiri na wasioogopa vitisho
9. Ni welevu
Marejeo
Arnold, Bernd. (Steuer und Lohnarbeit im Südwesten von Deutsch- Ostafrika,1891 bis 1916)
Bauer, Andreus. (Raising the Flag of War)
Charsley, S.R. (The Princes of Nyakyusa)
Ileffe, John. (A Modern History of Tanganyika)
Merensky, A. (Deutsche Arbeit am Nyaßa)
Oliver, Roland. (Sir Harry Johnston & the Scramble for Africa)
Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Wanyakyusa kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.